Swahili Resources

​​​Ofisi ya Matumizi ya Lugha – Wakalimani na Watafsiri

Mahakama ya Haki ya Kentucky imejizatiti kuhakikisha upatikanaji sawa wa haki kwa watu wote waliokuja mahakamani kwetu bila gharama, bila kujali lugha wanayoizungumza. Ofisi ya Matumizi ya Lugha (Office of Language Access, OLA) inatoa huduma ya matumizi ya lugha katika lugha zaidi ya 80 kila mwaka.

Mahakama za mashtaka ya ndani zina wajibu wa kuratibu wakalimani kwa ajili ya masikizo ya mahakama. Ikiwa wewe au mtu unayemfahamu anahitaji kumtumia mkalimani, tafadhali wasiliana na mahakama ambayo masikizo yatafanyika. Kupata taarifa za mawasiliano za mahakama ya eneo lako au Kalani wa Mahakama ya Mzunguko, chagua wilaya yako kwenye menyu kunjuzi katika kisanduku cha buluu juu ya ukurasa huu (“Select a County”).

Mkalimani wa mahakama anapaswa kutafsiri kikamilifu na kwa usahihi kile kilichoelezwa au kilichoandikwa. Mkalimani hapaswi kamwe kubadilisha, kufupisha, kuondoa, au kuongeza chochote wakati anapotafsiri. Mkalimani hapaswi kamwe kuelezea maana ya kile kilichoelezwa au kilichoandikwa, wala mkalimani hapaswi kutoa ushauri wa kisheria au kuwa wakili wa mahakama au upande wowote.

Waathirika wa ukatili na unyanyasaji wa majumbani (vilevile ukatili na unyanyasaji wa mahusiano), shambulio la kingono, au unyemeleaji wanaweza kuomba amri ya ulinzi kutoka mahakamani. Fomu hizo hizo za kisheria hutumika kwa ajili ya ukatili wa majumbani na amri za ulinzi kati ya mtu na mtu (ukatili wa mahusiano). Hizi zinajumuisha Ombi/Pendekezo la Amri ya Ulinzi na Pendekezo la Kurekebisha Amri ya Awali ya Ulinzi. Unaweza kuzipakua fomu hizi hapo chini au unaweza kuzichukua kwenye Ofisi ya Karani wa Mahakama katika wilaya ambayo unaishi (au ambayo umekwenda ili kujinusuru kutendewa ukatili). Kwa taarifa za mawasiliano bofya hapa.

Msaada wa matumizi ya lugha utatolewa kwa waombaji wenye ufahamu mdogo wa Kiingereza ili kuwasaidia kujaza na kuwasilisha fomu muhimu. Tafsiri za fomu hizi na nyingine za mahakama zinapatikana kwa lugha chache za kigeni kwa lengo la taarifa tu na haziwezi kuwasilishwa mahakamani. Fomu pekee ambazo mahakama itazikubali ni fomu rasmi za lugha ya Kiingereza.

Kupata taarifa zaidi tembelea Ukurasa wa Taarifa ya Amri za Ulinzi, au soma chapisho lifuatalo: Jinsi ya Kupata Amri ya Ulinzi

Pakua fomu kwa muundo wa PDF:

AOC-275.1 Ombi/Pendekezo la Amri ya Ulinzi

AOC-275.6 Pendekezo la Kurekebisha Amri ya Awali ya Ulinzi

​Mpango wa Huduma ya Kabla ya Mashtaka wa  Kentucky unaendeshwa chini ya mkataba, unaoungwa mkono na katiba ya nchi na ya shirikisho, kwamba washtakiwa wanachukuliwa kutokuwa na hatia hadi wanapothibitika kuwa na hatia na wana haki ya kupata dhamana inayostahiki. Washtakiwa wana haki ya kupewa masharti machache ya kuachiliwa huru kadri iwezekanavyo, kutegemeana na iwapo wanaweza kufika mahakamani na kama wanahatarisha usalama wa umma.

​Wafanyakazi wateule wa mahakama (Court Designated Workers, CDWs) wanashughulikia malalamiko ya vijana na watoto dhidi ya watu wenye umri chini ya 18. Malalamiko yanajulikana kama uvunjifu wa sheria au makosa ya watoto. Makosa ya watoto ni aina ya tabia za watoto ambazo si uhalifu, kama vile kutoroka nyumbani, kutohudhuria darasani, matumizi ya tumbaku au kuonyesha utukutu nyumbani au shuleni. Uvunjifu wa sheria ni sawa na uhalifu wa watu wazima.

Uhalifu sugu zaidi na wahalifu wanaorudia hupelekwa kwenye mahakama za kawaida. Vijana au watoto waliojihusisha na makosa madogo wanastahiki kijumla kuingia kwenye makubaliano mbadala. Makubaliano mbadala ni mikataba ya hiari kati ya CDW na mtoto/kijana ili kusuluhisha malalamiko, na ina masharti ambayo yanahusiana na uhalifu/makosa ya watoto na mara nyingi yanajumuisha moja au zaidi ya yafuatayo:

Rudisho
Huduma ya Jamii
Amri ya kutotembea
Unasihi
Kuhudhuria Semina za Elimu
Uchunguzi wa Dawa za kulevya/Pombe

Mchakato wa hukumu mbadala umeandaliwa kuelimisha, kufundisha fikra za uwajibikaji, na kuzuia watoto kuingia kwenye matatizo zaidi. CDWs (TRANSLATOR: LEAVE AS “CDWs”) zinafuatilia makubaliano mbadala, ambayo yanaweza kuwepo hadi miezi sita, ili kuhakikisha kwamba vijana/watoto wanatii masharti. Ikiwa kijana/mtoto anakamilisha kwa ufanisi makubaliano, kesi inatupiliwa mbali. Ikiwa sivyo, kesi inapelekwa kwenye mahakama za kawaida.

Kupata taarifa za mawasiliano za mahakama ya eneo lako au Kalani wa Mahakama ya Mzunguko, chagua wilaya yako kwenye menyu kunjuzi katika kisanduku cha buluu juu ya ukurasa huu (“Select a County”). (kwa Kiingereza)

Mchakato wa Malalamiko ya Matumizi ya Lugha​​

Kadi ya NAZUNGUMZA (PDF inayopakulika hapa)

Ionyeshe kwa karani ili kuomba mkalimani.

Mkalimani wa mahakama anaweza kukusaidia iwapo unaomba huduma ya moja kwa moja mahakamani. Hata hivyo, tambua kwamba hawezi kukusaidia katika huduma isiyo ya mahakama, ikiwemo kuzungumza faragha na wakili wako.

Fomu za mahakama zilizotafsiriwa - Kwa madhumuni ya kufahamisha pekee.  Fomu katika lugha nyinginezo kando na Kiingereza hazitakubaliwa na  mahakama. Ni fomu za Kiingereza tu zitakubaliwa. Tafadhali kumbuka kwamba Fomu za Kumbukumbu zipo kwa Kiingereza, lakini zinaweza kuchujwa kwa lugha.

Jinsi ya Kupata Amri ya Ulinzi

Faharasa za maneno ya kawaida ya kisheriaMahakama ya Haki ya Kentucky haijaidhinisha au haijatoa hakikisho la huduma kwa kuunganishwa kwenye shirika katika tovuti hii.

​Sisi hapa katika Ofisi ya Matumizi ya Lugha tunajivunia wenyewe kwa kutoa huduma kiwango cha juu kadri iwezekanavyo kwa wale wanaotumia huduma zetu. Ikiwa ungependa kutueleza uliyopitia hivi karibuni na mmoja wa wakalimani wetu, au ikiwa unahitaji taarifa zaidi kuhusiana na matumizi ya lugha katika mahakama za Kentucky, tafadhali tumia muda wako kidogo kujaza fomu ya mtandaoni hapo chini, ili mwakilishi kutoka idara yetu aweze kuwasiliana na wewe hapo baadaye. Tunatarajia kuzungumza na wewe punde!

Contact Us

Hapo chini utaona viunganishi mbalimbali muhimu vinavyohusiana na upataji wa huduma ndani ya Mahakama ya Haki ya Kentucky. Ingawa baadhi ya taarifa zinaweza kupatikana katika lugha yako, viunganishi vilivyotolewa hasa vinakuongoza kwenye maudhui ya Kiingereza. Kuhakikisha kivinjari chako kinaonyesha matini katika lugha yako, hata hivyo kunaweza kusaidia. Mahakama ya Haki ya Kentucky haitoi hakikisho la ubora wa tafsiri iliyotolewa na kivinjari chako.

Tafuta msaada wa kubadilisha mipangilio ya lugha kwa Chrome hapa.